Muhtasari wa Tafiti Tano za Kaya Kufuatilia Idadi ya Watu waliofikiwa na Matokeo ya Afua za Malaria Tanzania, 2007-2008
sr-09-59.pdf — PDF document, 1,417 kB (1,451,250 bytes)
Author(s): Foreit KGF, Patton EG, Walker DM
Year: 2009
Abstract:Taarifa hii inatoa muhtasari wa matokeo makuu ya tafiti tano huru za kaya kuhusu afua za malaria zilizofanywa Tanzania Bara kati ya Oktoba 2007 na Septemba 2008. Mwezi Novemba 2008, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Malaria (PMI) waliitisha mkutano wa siku mbili, Dar es Salaam kuwezesha uwasilishaji wa njia na matokeo ya tafiti zote tano. Tafiti za Kaya ni muhimu sana katika mazingira ya ugonjwa wa malaria kwa ajili ya kupima kufikiwa na afua zilizolenga ngazi ya Kaya, kama vile vyandarua vyenye dawa (ITN) na katika kuelewa mielekeo ya matumizi ya mbinu za kuzuia malaria miongoni mwa walengwa. Kila utafiti ulichunguza jukumu mahususi la wakati ulipopangwa na kutekelezwa mwaka 2007-2008. Hata hivyo katika ari ya juhudi za Kupunguza Kasi na athari za Malaria ili kuboresha uwianishaji wa utafiti mkubwa wa Kaya, NMCP na PMI viliwakutanisha watafiti wa tafiti tano zilizohusika kujadili matokeo katika mkutano wa wazi. Matokeo yaliyomo katika chapisho hili la muhtasari yanayonyesha idadi ya vatu waliofikiwa na data za matokeo mara baada ya kampeni ya kitaifa ya usambazaji bure vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu (LLINS) kwa watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano (iliyozinduliwa rasmi, Mei, 2009) na kampeni nyingine kwa ajili ya usambazaji bure wa LLINS kwa kaya zote zilizobaki (inakadiriwa kuzinduliwa mwanzoni mwa 2010). Chapisho hili linakusudiwa kuwa kama chapisho moja la chanzo cha taarifa ya matokeo muhimu kutoka tafiti zote tano. Maelezo mahususi yanayohusu njia za utafiti (ikiwemo utayarishaji wa sampuli na dodoso), matokeo mengi zaidi yatafuatiliwa katika taarifa kamili za kila utafiti unaohusika.